Mwezi huu wa Septemba, viongozi wa mataifa ya dunia watajitolea kutimiza Malengo ya Ulimwengu kwa Maendeleo Endelevu ili kutimiza masuala matatu muhimu kufikia mwaka 2030. Kukomesha umaskini uliokithiri. Kupambana na ukosefu wa usawa na dhuluma. Kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Malengo ya Ulimwengu kwa maendeleo endelevu yanaweza kufanikisha masuala haya matatu. Katika nchi zote. Kwa watu wote.

Lakini Malengo haya hayawezi kutimizwa ikiwa watu hawayajui.

Kutoka tarehe 24 Septemba hadi tarehe 1 Oktoba, kila mtu kutoka kila dini, kila jamii, kila mahali, anaweza kushiriki katika Sala kwa Kila Mtu kwa kusambaza Malengo ya Ulimwengu kwa jamii yao ya waumini na marafiki zao.
Tunakualika kujiunga nasi na kupigia debe Malengo haya kupitia mafundisho na mambo unayoyafanya mara kwa mara katika dini yako.

Toa #Sala kwaKilaMtu na Sema na wote kuhusu dunia unayotaka kuiona kufikia mwaka 2030.

 

Kituo cha Nyenzo

Tafuta zana za kueneza taarifa kuhusu Malengo ya Ulimwengu na uyazungumzie katika jamii yako.

Angalia

Join us!

Tunangependa kujua wewe ni nani, upo wapi, na ni vipi unashiriki katika kampeni hii. Ongeza jina lako kwa orodha ya watu binafsi, mashirika, na jamii zinazoshiriki katika Sala kwa Kila Mtu ulimwenguni kote. (Majina hayatashirikiwa hadharani)